#HABARI: Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ameeleza kuwa serikali itaendelea kushirikiana na Jumuiy…

#HABARI: Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ameeleza kuwa serikali itaendelea kushirikiana na Jumuiy…

#HABARI: Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ameeleza kuwa serikali itaendelea kushirikiana na Jumuiya ya Taasisi za Elimu ya Juu (TAHLISO) kama wadau muhimu wa elimu, ili kuhakikisha kunakuwa na chachu ya mabadiliko na yenye tija katika elimu na Maendeleo ya nchi kwa ujumla.

Amebainisha hayo leo katiaka maadhimisho ya miaka 21 ya TAHLISO akiwa ni mgeni rasmi wa maadhimisho hayo.

Aidha ameeleza kuwa serikali imefanya mageuzi makubwa ya kisera, kisheria na kanuni huku ikifanya maboresho ya mitaala pamoja na sera ya mafunzo ya mwaka 2014 toleo la 2023 iliyozinduliwa Dkt.Samia samia tarehe 1 Februari 2025.

Maboresho hayo yanalenga kutatua changamoto za elimu na kuendana na mahitaji ya kitaifa kikanda na kimataifa, na mabadiliko haya yanakwenda kutoa elimu inayozingatia ujuzi unaohitajika katika soko la ajira na Maendeleo ya Taifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *