#HABARI: Viongozi wa Kata ya Karabagaine iliyoko ndani ya Halmashari ya Wilaya Bukoba, mkoani Kagera kwa kushirikiana na baadhi ya wananchi wa Kata hiyo wamefanikiwa kuwakamata watu sita wanaosadikiwa kuwa ni raia wa nchi ya Burundi waliokuwa miongoni mwa watu wengine 13 waliokutwa wamejificha Kichakani.
Hayo yamebainishwa na Afisa Mtendaji wa Kata ya Karabagaine, Beatrice Shangwe ambaye alishiriki zoezi la kuwakamata watu hao na badae kuwakabidhi kwa vyombo vya ulinzi na usalama.
#Follow @radioonetanzania
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.