#HABARI: Idara ya polisi nchini Kenya imeomba radhi Wakenya kufuatia tukio ambalo mahabusu aliyekuwa na ujauzito Milka Wangari a…

#HABARI: Idara ya polisi nchini Kenya imeomba radhi Wakenya kufuatia tukio ambalo mahabusu aliyekuwa na ujauzito Milka Wangari a…

#HABARI: Idara ya polisi nchini Kenya imeomba radhi Wakenya kufuatia tukio ambalo mahabusu aliyekuwa na ujauzito Milka Wangari alipoteza ujauzito kwenye selo za polisi baada ya kukamatwa kwa kosa la kuchukua shillingi elfu 9 za Kenya za mwajiri wake Joseph Gatuitha. Ripoti zikieleza kwamba polisi katika kituo hicho walikatalia mbali kumpeleka hospitalini mahabusu huyo licha ya kulalama kuwa alikuwa na maumivu. Mahabusu huyo alipatikana asubuhi kwenye seli za polisi akiwa amepoteza ujauzito wake.

Tayari Afisa mkuu wa kituo cha polisi cha Rwanyambo kaunti ya Nyandarua amesimamishwa kazi huku mamlaka ya kuangazia utendakazi wa polisI ikianzisha uchunguzi.

Kamanda wa polisi kaunti ya Nyandarua Stella Cherono amezuru kituo hicho cha polisi na kuomba radhi akiahidi kuchukuliwa hatua kwa waliohusika.Tukio ambalo limeibua ghadhabu kubwa nchini Kenya.

Tukio hili linajiri huku mamlaka ya kuangazia utendakazi wa polisi zikiliambia bunge la Kenya kwamba mahabusu 20 wamefariki kwenye selo za polisi ndani ya miezi minne iliyopita yakiwemo mauaji ya Albert Omondi Ojwang aliyepoteza kifo katika kituo cha Polisi cha Central jijini Nairobi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *