#HABARI: Waziri wa Katiba na Sheria Dkt

#HABARI: Waziri wa Katiba na Sheria Dkt

#HABARI: Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro ametaja mabadiliko 15 ya sheria ya Uchaguzi yaliyofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kuimarisha demokrasia na utawala bora nchini.

Waziri Ndumbaro amebainisha hayo mjini Tarime, mkoani Mara, alipokuwa akifungua mafunzo ya elimu ya kisheria kwa viongozi wa kata, ambapo amesema mabadiliko hayo yanadhihirisha dhamira ya kweli ya Rais Samia ya kujenga mfumo huru, wazi na wa haki wa uchaguzi.

Amesema mabadiliko hayo yamejumuisha kufutwa kwa sheria ya zamani ya uchaguzi ya taifa na ile ya Serikali za Mitaa, na badala yake kutungwa sheria mpya ya uchaguzi inayoendana na matakwa ya sasa ya kidemokrasia.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *