#HABARI: Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kupitia Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi, wamepiga kambi katika Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya matumizi bora ya Ardhi.
Elimu hiyo kwa awamu ya kwanza itatekelezwa katika vijiji vya Mpumbe, Mchenga Nyumba, Mpara, Mtawilile, Mitope, Mmawa, Mtimbo na Mipawa.
Na awamu ya pili itapita katika vijiji vya Mbangala, Chinokole, Mandarawe, Makanjiro, Nachinyimba, Kipindimbi, Nangurugai na Liugulu.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania