#HABARI: Katika kuhakikisha elimu ya nishati safi ya kupikia inamfikia kila Mtanzania, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Bw

#HABARI: Katika kuhakikisha elimu ya nishati safi ya kupikia inamfikia kila Mtanzania, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Bw

#HABARI: Katika kuhakikisha elimu ya nishati safi ya kupikia inamfikia kila Mtanzania, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Bw. Lazaro Twange, ametumia sehemu ya ziara yake ya kukagua maendeleo ya miradi ya umeme katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa, katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupika kwa umeme kwa viongozi wa Serikali za Mikoa na Wilaya ili kuongeza uelewa zaidi kwa wananchi.

Bw. Twange ametumia nafasi hiyo kuelimisha na kutoa zawadi za majiko janja yenye teknolojia inayotumia umeme kidogo kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Kenani Kihongosi, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Saidi Mtanda, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe. Amina Makilagi Pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Wakili Julius Mtatiro ikiwa ni sehemu ya Kampeni ya TANESCO ya kuendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa kutumia umeme.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *