#HABARI: Serikali ya Mkoa wa Tabora, imekamilisha uchunguzi wa tukio la mwanafunzi wa kidato cha tano Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Tabora, ambaye utambulisho wake umehifadhiwa aliyesoma shuleni hapo akiwa na ujauzito bila ya uongozi wa shule kujua kisha akajifungua mtoto bila usaidizi wa mtu yeyote kwenye vyoo vya hospitali ya rufaa ya mkoa huo Kitete wakati alipokuwa akipatiwa matibabu ya kichwa na mguu.
Uchunguzi huo umebaini matukio mbalimbali yakiwemo uzembe wa uongozi wa shule hiyo ulioshindwa kusimamia taratibu na miongozo ya elimu nchini ambapo walimu wa shule hiyo wamedai hawakuwahi kujua kama mwanafunzi wao ana ujauzito katika kipindi chote za miezi tisa.
Akizungumza mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Usalama ya Mkoa wa Tabora, wazazi na uongozi wa shule hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama ya Mkoa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Bw. Paulo Chacha, mbali na kukemea tukio hilo lakini pia amelitaka Jeshi la Polisi kuhakikisha wanamkamata na kumchukulia hatua za kisheria aliyehusika na ujauzito wa mwanafunzi huyo.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania