#HABARI: Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Bw. Lazaro Twange amesema Mradi wa uzalishaji umeme unaotokana na jua wa Kishapu mkoani Shinyanga umefikia asilimia 63.3 kukamilika ambapo amesema awamu ya kwanza ya Mradi huo utazalisha Megawati 50 ambazo zitaingizwa kwenye gridi ya Taifa ifikapo mwishoni mwa mwezi wa kumi mwaka huu.
MD Twange ameyasema hayo alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi huo ambao unagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 118 kwa awamu ya kwanza huku awamu ya pili ikitarajia kutumia kiasi cha shilingi Bilioni 204.
“Kwanza tunamshukuru Mhe. Rais kwa kutupatia fedha kwa awamu zote, kama mnavyoona kazi inaendelea na Mradi unatarajia kuingizwa kwenye Gridi ya Taifa mwishoni mwa mwezi wa kumi kwa ajili ya kuwasambazia umeme wananchi, lakini pia tuko katika hatua za mwisho za manunuzi kwa ajili ya kumpata mkandarasi atakayetekeleza Mradi kwa awamu ya pili ambayo itazalisha megati 100,” alisisitiza Mkurugenzi Mtendaji Twange.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania