#HABARI: Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ngwala, iliyopo Kata ya Ngwala, wilayani Songwe, mkoani Songwe, wameondokana na adha ya uhaba wa vyumba vya madarasa uliokuwa ukisababisha msongamano mkubwa wa wanafunzi madarasani, baada ya wazazi kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo Kampuni ya Mamba Minerals, kujenga vyumba viwili vya madarasa ya kisasa, chumba cha maktaba pamoja na ofisi ya walimu, nakuifanya shule hiyo kuwa na jumla ya vyumba sita vya kusomea.
Meneja Uhusiano wa Kampuni hiyo inayotarajia kuanza uzalishaji wa madini adimu duniani ya Rare Eath, yaliyogunduliwa katika Kata hiyo, Bi. Marry Duncan, amesema tangu mwaka 2024 mpaka mwaka 2025, wamekeleza jumla ya miradi mikubwa minne ya kijamii ikiwemo ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa pamoja na maktaba ya kisasa, uliogharimu kiasi cha shilingi milioni mia moja na nane, huku mkakati uliopo ni kuifanya shule hiyo kuwa ya kisasa na ya mfano katika eneo hilo kwa kuongezea miundo mbinu mingine ikiwemo mabweni pamoja na viwanja vya michezo.
#itvdigital #itvupdates #itvtanzania.
#follow @radioonetanzania