#HABARI: Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe

#HABARI: Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe

#HABARI: Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango, leo tarehe 07 Juni 2025 ameondoka nchini kuelekea Ufaransa, kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano wa Tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Bahari (UNOC3), utakaofanyika Jijini Nice, kuanzia tarehe 09 hadi 13 Juni, 2025.

UNOC3 ni jukwaa muhimu la kimataifa la kuhamasisha utekelezaji wa Lengo la Maendeleo Endelevu namba 14 (SDG 14) linalolenga kuhifadhi na kutumia kwa uendelevu rasilimali za bahari, bahari kuu na mazingira ya pwani.

Mkutano huo unawakutanisha Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, Mashirika ya Kimataifa, Asasi za Kiraia pamoja na Sekta binafsi.

Aidha, Makamu wa Rais anatarajiwa kushiriki katika Mikutano ya Uwili yenye lengo la kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania, Mashirika na Mataifa yanayoshiriki Mkutano huo.

Mkutano huo utasaidia kuimarisha nafasi ya Tanzania kimataifa, kujenga ushirikiano mpya na kuhamasisha upatikanaji wa rasilimali kwa ajili ya maendeleo ya uchumi wa buluu.

#itvdigital #itvupdates #itvtanzania.

#follow @radioonetanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *