#HABARI: Rais wa Marekani, Donald Trump, amerudisha marufuku ya safari kwa raia kutoka nchi 12, nyingi zikiwa za Afrika na Mash…

#HABARI: Rais wa Marekani, Donald Trump, amerudisha marufuku ya safari kwa raia kutoka nchi 12, nyingi zikiwa za Afrika na Mash…

#HABARI: Rais wa Marekani, Donald Trump, amerudisha marufuku ya safari kwa raia kutoka nchi 12, nyingi zikiwa za Afrika na Mashariki ya Kati. Hatua hii inaanza kutumika kuanzia Jumatatu ijayo.

Miongoni mwa nchi zilizopigwa marufuku kuingia Marekani ni Afghanistan, Iran na Somalia. Raia wa mataifa haya hawataruhusiwa kuingia Marekani kwa sababu za usalama, kwa mujibu wa taarifa ya kampeni ya Trump.

Aidha, nchi kama Burundi, Cuba na Laos zimewekewa vizuizi vya visa, ambavyo vinazuia uhamiaji wa kudumu pamoja na visa za wanafunzi na watalii.

Sera hii ni mwendelezo wa marufuku ya safari ambayo Trump aliwahi kuiweka wakati wa muhula wake wa kwanza akiwa rais.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *