KICHAPO ilichopewa UDSM Outsiders kutoka kwa KIUT cha pointi 65-60, kimeifanya timu hiyo ishuke katika uongozi wa msimamo wa Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL) hadi kwenda nafasi ya tano ikiipisha kileleni ABC.
Kushuka kwa Outsiders kumeifanya ABC iongoze Ligi hiyo kwa pointi 12, ikifuatiwa na Dar City iliyopata pointi 10.
Takwimu za msimamo wa Ligi hiyo zimeonyesha Stein Warriors imeshika nafasi ya tatu kwa pointi 10, Pazi (10), UDSM Outsiders (9), Mchenga Star (9), JKT (8), Vijana ‘City Bulls’ (8) na KIUT (7).
Nyingine ni DB Oratory (7), Chui (7), Polisi (7), Savio (6), Kurasini Heat (6), Srelio (6) na Mgulani JKT (5).
MSIMAMO (WANAUME)
TIMU PLD W L PTS
ABC 6 6 0 12
Dar City 5 5 0 10
Stein Warriors 6 4 2 10
Pazi 5 4 1 9
UDSM 5 4 1 9
Mchenga Stars 6 3 3 9
JKT 5 3 2 8
Vijana 5 3 2 8
KIUT 5 2 3 7