#HABARI: Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Victoria Mwanziva, amewataka Viongozi wa Vyama vya Msingi vya Ushirika (AMCOS) kuwa na lugha mzuri kwa wakulima pindi wanapoombwa kuelekeza jambo na si kuwafokea.
Mwanziva ameyasema hayo katika kikao kazi kilichoandaliwa na Chama Kikuu cha Ushirika Lindi Mwambao na kuwakutanisha Wajumbe wa Bodi, Mameneja, Makarani, Watunza Mizani na Maghala pamoja na Wadau kutoka Taasisi za Fedha.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania