#HABARI: Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya za mafuta kwa mwezi Juni 2025, zikionyesha…

#HABARI: Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya za mafuta kwa mwezi Juni 2025, zikionyesha…

#HABARI: Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya za mafuta kwa mwezi Juni 2025, zikionyesha mabadiliko tofauti katika mikoa mbalimbali ya Tanzania.

Katika Jiji la Dar es Salaam, bei ya petroli imeshuka hadi Sh2,885 kwa lita kutoka Sh2,912, dizeli hadi Sh2,826 kutoka Sh2,859, huku mafuta ya taa yakibaki Sh2,877.

Mkoa wa Tanga, bei mpya ni:

Petroli Sh2,946

Dizeli Sh2,887

Mafuta ya taa Sh2,938

Lakini hali ni tofauti kwa Mtwara, ambapo bei zimepanda na kuwa za juu zaidi nchini:

Petroli Sh2,978

Dizeli Sh2,918

Mafuta ya taa Sh2,969

EWURA imeeleza kuwa bei za mafuta kimataifa zimepungua kwa wastani wa asilimia 0.9 kwa petroli, 3.4 kwa dizeli, na 3.7 kwa mafuta ya taa. Hata hivyo, gharama za uagizaji zimepanda, hasa kupitia Bandari ya Mtwara ambapo uagizaji wa petroli umeongezeka kwa hadi asilimia 51.55 hali iliyochangia kupanda kwa bei mkoani humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *