#HABARI: Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Dkt

#HABARI: Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Dkt

#HABARI: Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Dkt. Mwingulu Nchemba amesema, hadi kufikia Aprili, 2025 wizara imelipa kwa wakati shilingi bilioni 315.08 kama mafao ya kiinua mgongo kwa wastaafu na warithi wanaolipwa na Hazina.

Amesema, wizara ilifanya hivyo baada ya kupokea nyaraka kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ikiwa pia ni utekelezaji wa mipango yake kwa mwaka 2024/25.

Dkt.Nchemba ameyasema hayo leo Juni 4,2025 bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025|2026.

“Aidha, michango ya kisheria ya kila mwezi kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii iliwasilishwa kwa wakati na malipo ya kila mwezi ya pensheni ya mifuko ya hifadhi ya jamii yalifanyika kwa wakati baada ya kupokea hati za madai.”

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.

#Follow @radioonetanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *