#HABARI: Kufuatia Ofisi ya Msajili wa Jumuiya za Kiraia kulifutia usajili Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima ambaye pia ni Mbunge wa Kawe, hii leo ITV Digital imeshuhudia kanisa hilo likiwa limezungushiwa utepe chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi huku baadhi ya waumini wa kanisa hilo wakiwa nje.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msajili wa Jumuiya za Kiraia Emmanuel Kihampa Juni 2, mwaka huu, kufutwa kwa kanisa hilo ni kutokana na mahubiri yenye nia ya kuchonganisha wananchi na Serikali yanayoashiria uvunjifu wa amani ya nchi yaliyotolewa na Askofu Gwajima.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania