#HABARI: Waziri wa Katiba na Sheria Mhe

#HABARI: Waziri wa Katiba na Sheria Mhe

#HABARI: Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema kuwa, Sheria za Nchi haziendi likizo wakati wa kampeni za Uchaguzi bali zinakuwepo na kila Mwananchi anapaswa kuzitii kama inavyotakiwa.

Dkt. Ndumbaro ameyasema hayo wakati akifungua Mafunzo ya sita ya Mawakili wa Serikali zaidi ya 600 kutoka Wizara, Taasisi na Mamlaka mbalimbali za Umma .

“Mwaka huu ni mwaka wa Uchaguzi, kuna mengi tutayasikia, lakini katika kipindi hiki cha Kampeni mimi hua najiuliza sana, hivi Sheria zinakwenda likizo? Kwa sababu tunataka kuaminishwa uvunjifu wa Sheria utakaotokea kipindi cha Kampeni sio uvunjifu wa Sheria kwa sababu tu unafanywa na wanasiasa. Kwa uelewa wangu wa Sheria nasema kipindi cha Kampeni Sheria haziendi likizo, Sheria zipo zinafanya kazi, Wanasheria wapo wanafanya kazi, Mahakama zipo zinafanya kazi,” amesisitiza Dkt Ndumbaro.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.

#Follow @radioonetanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *