#HABARI: Siku moja baada ya ITV Digital kutoa taarifa za wazazi wa mtoto aliyezaliwa bila sehemu ya haja kubwa, wakazi wa Kata ya Isevya Manispaa ya Tabora ambao wameshindwa kumudu gharama za matibabu ya mtoto huyo pamoja na kukosa fedha za kujikimu, Serikali ya Mtaa wa Bombamzinga katika kata hiyo imetekeleza maelekezo ya Naibu Waziri wa Afya Daktari Godwin Mollel ya kuthibitisha hali duni ya wazazi hao ili wakapate matibabu bila malipo katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando iliyopo jijini Mwanza.
Kwa sasa mtoto huyo anapitia changamoto ya kutoa haja kubwa kupitia eneo la tumbo alilotobolewa kwa dharura na inahitajika huduma nyingine ya matibabu ya kuziba utumbo huo ili kuruhusu eneo sahihi la kujisaidia lifanye kazi ambapo wazazi wake wamewaomba wasamaria wema kuwasaidia gharama za matibabu pamoja na fedha za kujikibu kupitia nambari za simu za +255789218200 jina ni Rajabu Mabula ambaye ni Baba Mzazi.
Hata hivyo, ITV Digital ilimtafuta Naibu Waziri wa Afya Daktari Godwin Mollel kuona namna bora ya kumsaidia mtoto huyo kwa haraka ambapo alielekeza Serikali ya Mtaa wa Momba Mzinga kuthibitisha hali duni ya familia hiyo ili Serikali ibebe gharama zote za matibabu ya mtoto huyo jambo ambalo limefanikiwa kwa siku ya leo Juni 3, 2025.
Aidha, mbali na familia hiyo kuishuku Serikali na ITV Digital kwa kutangaza changamoto zao hadi kuanza kupata msaada lakini pia wameendelea kuiomba jamii kuendelea kuwasaidia fedha za kujikimu katika nyakati hizi za matibabu ya mtoto wao.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania