#HABARI: Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amesema kitabu alichoandika Alhaj Mzee Mohamed Mustafa Songambele, kitakuwa mojawapo ya rejea adhimu za historia ya Tanzania.
Balozi Nchimbi amesema kuwa kitabu hicho kiitwacho “Safari ya Karne”, kina utajiri wa maelezo kuhusu mapambano ya kutafuta uhuru wa Tanganyika, kupatikana kwa nchi na taifa la Tanzania na kuundwa kwa CCM.
Dkt. Nchimbi amesema hayo alipokuwa akitoa salaam za pole na rambirambi kwenye msiba wa Hayati Alhaji Mzee Songambele, akimwakilisha Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, mjini Songea, mkoani Ruvuma.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania