#MICHEZO: Maandalizi ya Maonesho ya Kimataifa ya Utalii karibu, Killi Fair yanayo tarajiwa kuanza Juni 6 Jijini Arusha, yamefikia asilimia 75 huku zaidi ya Makampuni miatano kutoka zaidi ya nchi arobaini yakidhibitisha kushiriki kutangaza vivutio vya utalii wa Tanzania.
Akikagua maandalizi ya ujenzi wa eneo litakalo tumika kwa maonesho hayo, zaidi ya kampuni 500 kutoka zaidi ya nchi 40 zimeshathibitisha kushiriki kwa lengo la kuonyesha mnyororo wa thamani katika sekta ya utalii na kusaidia kukuza uchumi wa wananchi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni ya KiliFair, Dominic Shoo, amesema maonesho ya mwaka huu yameboreshwa zaidi na yatafanyika kwa viwango vya juu ikilinganishwa na miaka iliyopita.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania