#HABARI: Serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania (TRC) imekamilisha upembuzi yakinifu kwa ajili ya Ujenzi wa Reli ya Kisasa ka…

#HABARI: Serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania (TRC) imekamilisha upembuzi yakinifu kwa ajili ya Ujenzi wa Reli ya Kisasa ka…

#HABARI: Serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania (TRC) imekamilisha upembuzi yakinifu kwa ajili ya Ujenzi wa Reli ya Kisasa katika Jiji la Dodoma (Dodoma Commuter Train).

Kauli hiyo ya Serikali imetolewa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile ambaye amesema Ujenzi wa Reli hiyo unalenga kuimarisha usafiri katika Jiji la Dodoma kwa kuunganisha Jiji na viunga vyake ikiwemo Kiwanja cha Ndege
cha Kimataifa Msalato.

Mheshimiwa Kihenzile amesema Serikali ipo katika hatua za utafutaji wa rasilimali fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa reli hiyo.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.

#Follow @radioonetanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *