#HABARI: Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Songwe, Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi (SSP) Joseph Bukombe, amewataka madereva wa magari ya serikali yakiwemo ya viongozi mkoani humo kuhakikisha wanafuata sheria za usalama barabarani nakuijiepusha na mwendokasi hasa katika maeneo yasiyoruhusiwa ili kuepusha ajali ambazo zimekuwa zikisababisha vifo, ulemavu wa kudumu pamoja na uharibifu wa magari ya serikali.
Kamanda Bukombe, ametoa rai hiyo alipokutana na madereva zaidi ya hamsini wa serikali mkoani humo katika mafunzo maalum yaliyoandaliwa na kikosi hicho ambayo yamelenga kutoa elimu sambamba na kuwakumbusha majukumu yao pindi wanapokuwa na viongozi ambao wamekuwa wakiwasikiliza badala ya kufuata sheria.
Aidha madereva hao wametakiwa kuwa washauri wa viongozi pamoja na wakuu wa idara wanaowaendesha pindi wanapojisikia hali ya uchovu na usingizi wakiwa safarini nakuomba muda wa kupumzika hali ambayo itasaidia kuepusha ajali .
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania