#HABARI: Kufuatia nyumba ya Muhudumu wa Afya katika Zahanati ya Simbanguru katika Kata ya Nkonko wilayani Manyoni, kubomolewa na Tembo zaidi ya miaka mitatu, wananchi zaidi ya 10,000 wanaohitaji huduma za afya nyakati za usiku, wanalazimika kumfuata muhudumu huyo umbali mrefu, jambo ambalo ni hatari kupoteza maisha kwa wagonjwa na hasa wakinamama waja wazito kwa kuchelewa kupata huduma.
Kutokana na hali hiyo Mamlaka ya uhifadhi wa Wanyamapori Tanzania Kanda ya Kati tawa imetoa mifuko ya saruji 90 kwa ajili ya ukarabati wa nyumba hiyo.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania