#HABARI: Ilani mpya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kipindi cha 2025–2030, imeelezwa kuwa dira ya maendeleo Jumuishi kwa Watanzania, ikilenga kuchochea uchumi wa kisasa, kuongeza ajira, kuboresha huduma za jamii na kuimarisha nafasi ya Tanzania kimataifa kupitia Diplomasia ya Uchumi.
Afisa wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Abdallah Kirungu, ambaye pia aliwahi kuwa Afisa Mwandamizi Mkuu wa Ubalozi Mdogo wa Tanzania Dubai, amesema Ilani hiyo imejikita katika maeneo yote muhimu ya maisha ya Mtanzania, yakiwemo elimu, afya, maji, kilimo, miundombinu, ulinzi na usalama, michezo, na utamaduni.
Kwa mujibu wa Kirungu, moja ya maeneo yaliyopewa uzito mkubwa ni Diplomasia ya Uchumi, ambapo amesema kuwa ilani hiyo inalenga kukuza ushirikiano wa kikanda na kimataifa ili kutetea maslahi ya Taifa na kuongeza uwekezaji.
Bofya hapa.-https://www.itv.co.tz/news/ilani-ya-ccm-kumulika-diplomasia-ya-uchumi