#HABARI: Mabasi nane ya abiria yanayofanya safari zake ndani na nje ya mkoa wa Songwe, yamezuiliwa kuendelea na safari baada y…

#HABARI: Mabasi nane ya abiria yanayofanya safari zake ndani na nje ya mkoa wa Songwe, yamezuiliwa kuendelea na safari baada y…

#HABARI: Mabasi nane ya abiria yanayofanya safari zake ndani na nje ya mkoa wa Songwe, yamezuiliwa kuendelea na safari baada ya kubainika kuwa na makosa mbalimbali ikiwemo ubovu na uchakavu wa matairi hali inayohatarisha usalama wa abiria huku mengine zaidi ya hamsini yakitozwa faini baada ya kubainika kuwa na makosa mbalimbali ikiwemo kutokutoa tiketi mtandao kwa abiria .

Akizungumza mara baada ya kuchukua hatua hiyo katika ukaguzi uliofanyika kwenye kituo kikubwa cha ukaguzi Chimbuya ambacho hutumika kukagua magari ya mizigo yanayoingia na kutoka nchini kupita mpaka wa Tunduma , Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoa waSsongwe (SSP) Joseph Bukombe amesema oparesheni hiyo imeanza tarehe 22 mwezi mei na itamalizika tarehe 22 mwezi june mwaka huu.

Kamanda Bukombe amesema baadhi ya magari ya abiria tairi zake zimekuwa ni vipara hali ambayo inahatarisha usalama wa abiria na watumiaji wengine wa barabara hivyo kama mamlaka hawana budi kuchukua hatua mapema ili kunusuru maisha ya watu wengine kwani mkoa wa songwe jiografia yake ni milima na mitelemko mikali hivyo hawataruhusu magari kuendelea kuwa na tairi vipara.

katika hatua nyingine kikosi hicho kimezuia leseni kumi na saba zilizokutwa na makosa mbalimbali huku magari zaidi ya hamsini yakipigwa faini kwa kukutwa na makosa mbalimbali ikiwemo baadhi kutokutoa tiketi mtandao , huku abiria wakitakiwa kupaza sauti pindi wanapobaini hali ya makosa kwenye vyombo hivyo vya usafiri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *