#HABARI: Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mkoa wa Shinyanga, imefanikiwa kuwabaini viongozi wa Chama cha Msingi cha Ushirika cha Ibambala Halmashauri ya Ushetu, wilayani Kahama, kufuja fedha kiasi cha shilingi milioni 151.5 ambazo ni sehemu ya fidia kwa wakulima wa zao la Tumbaku, walioathiriwa na mafuriko ya maji ya mvua na kukosa mavuno ya msimu wa mwaka 2023/20245.
Mkuu wa TAKUKURU, Mkoa wa Shinyanga Donasian Kessy, amebainisha hali hiyo wakati akitoa taarifa ya shughuli za TAKUKURU, ikiwemo uchunguzi wa miradi ya maendeleo kwa kipindi cha robo ya tatu ya mwaka 2024/2025 kilichoanzia mwezi Januari hadi Machi 2025.
Aidha, Mkuu wa TAKUKURU Bw. Kessy, amesema kiasi kilichodhibitiwa na kurudishwa na viongozi hao, baada ya kubainika ni shilingi milioni 92.16, ambapo malipo hayo yalikuwa ni sehemu ya fidia kwa wakulima waliopata hasara kutokana na mafuriko yaliyoharibu zao la Tumbaku kwenye mashamba yao.
Mkuu wa TAKUKURU Donasiani Kessy, amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Katibu Meneja wa Chama hicho Bw. Charles Alex Shiyengo na Mwenyekiti wake Bw. Faida Paulo Deda, ambapo wengine ni Bi. Lucy Masanja Gibabita Mke wa Katibu Meneja na Bw. Charles Charles Mtoto wa Katibu Meneja.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania