#HABARI: Wananchi mkoani Njombe wameshindwa kuficha hisia zao mara baada ya kupatiwa matibabu na kuamua kuhamasishana wao kwa wa…

#HABARI: Wananchi mkoani Njombe wameshindwa kuficha hisia zao mara baada ya kupatiwa matibabu na kuamua kuhamasishana wao kwa wa…

#HABARI: Wananchi mkoani Njombe wameshindwa kuficha hisia zao mara baada ya kupatiwa matibabu na kuamua kuhamasishana wao kwa wao kuhudhuria kambi ya Madaktari Bingwa wa Rais Samia inayoendea hivi sasa katika halmashauri zote za mkoa huo, kwani muda wa siku sita bado haujakamilika.

Akizungumza mara baada ya kupatiwa huduma katika Hospitali ya Halmashauri ya Njombe mji Kibena , Bw. Sufian Kihongosi (65) mkazi wa eneo hilo amesema wanashukuru uwepo wa madaktari hao, kwani wameweza kupatiwa huduma nzuri bila kulazimika kusafiri kusaka huduma hizo za Kibingwa.

“Nishukuru madaktari bingwa wamekuja eneo hili imekuwa jambo jema na nzuri, tunashukuru pia Serikali kwa kutuletea huduma karibu na maeneo yetu,” ameeleza. Bw. Kihongosi.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.

#Follow @radioonetanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *