#HABARI: Simba SC wamefanikiwa kufikisha alama 72, alama moja nyuma ya Wapinzani wao wa jadi, Yanga SC wenye alama 73.
Simba wamefanikiwa kufikisha alama hizo baada ya kupata ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Singida Black Stars katika mechi ya Ligi Kuu ya NBC iliyopigwa katika dimba la KMC Complex leo Mei 28, 2025.
Ushindi huo umeongeza presha ya ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC kufuatia Yanga kugomea mchezo wao wa kiporo dhidi ya Simba ambao umepangwa kupigwa Juni 15, mwaka huu.
Endapo watacheza Yanga, mechi hiyo ina asilimia kubwa ya kuamua ubingwa kati ya timu hizo mbili. Wasipocheza, Simba ana asilimia nyingi zaidi za kuwa bingwa msimu huu.
Simba na Yanga sasa wamelingana michezo 27, wamesalia na michezo 3 kila mmoja kabla ya kumaliza msimu 2024-25.
Vipi Yanga wataleta timu? Tupe maoni yako hapa chini.