#HABARI: Naibu Waziri wa Nishati Mhe Judith Kapinga amezindua rasmi kituo mama cha kujaza gesi asilia kwenye magari kilichopo ubungo eneo la mawasiliano Dar es Salaam chenye uwezo wa kujaza magari nane kwa wakati mmoja na magari elfu moja na mia mbili kwa siku jambo ambalo linatazamiwa kuondoa adha ya msongamano wa magari kwenye vituo vya kujaza gesi kutokana na uchache wa vituo hivyo.
Uzinduzi huo wa kituo mama cha kujaza gesi asilia kwenye magari, umeenda sambamba na uzinduzi wa basi jipya la majaribio la mwendokasi linalotumia gesi ambapo kwa kuanzia wananchi watapanda bure kwa sharti la kuwa na kadi za malipo na ruti yake itakuwa Morocco- Gerezani.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania