#HABARI: Waziri wa Maji Jumaa Aweso ametumia jukwaa la Bunge kuvipongeza vilabu vikubwa vya soka nchini- Simba Sports Club na Young Africans SC (Yanga) kwa mafanikio yao ya hivi karibuni kwenye mashindano ya kitaifa na kimataifa, akisisitiza kuwa mafanikio ya vilabu hivyo ni fahari kwa Taifa zima.
Akiwasilisha Bajeti ya Mageuzi ya Sekta ya Maji kwa mwaka wa fedha 2025/26, siku ya Alhamisi, Mei 8, 2025, Aweso ameanza kwa kunukuu andiko kutoka Biblia akisema: “Warumi 12:15 inasema, ‘Furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja nao waliao’. Hivyo, ninaomba kutumia fursa hii kuipongeza Timu ya Simba, Wekundu wa Msimbazi kwa kuingia fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.”
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania