#HABARI: Mafuriko yaliyoathiri kaya zaidi ya 300, na kutengeneza bwawa katika Mtaa wa Katubuka Manispaa ya Kigoma Ujiji, sasa ya…

#HABARI: Mafuriko yaliyoathiri kaya zaidi ya 300, na kutengeneza bwawa katika Mtaa wa Katubuka Manispaa ya Kigoma Ujiji, sasa yamevunja kingo na kujitengenezea njia kuelekea ziwa Tanganyika, hata hivyo mitaa yalipokatiza maji hayo nako yameacha athari kubwa kwa watu wanaoishi maeneo hayo.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Katubuka Bw. Shedrack Brushi, amesema kuwa kwa tathimini aliyofanya, maji hayo yameathiri kaya zaidi ya 60, katika maeneo ambayo maji hayo yamekatikiza kuelekea ziwa Tanganyika, hivyo inahitajika msaada mkubwa kwa waathirika hao.

Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu tayari imetoa msaada wa kibinadamu kwa kaya zilizoathirika hapo awali, huku mikakati ya kukomesha tatizo hilo ambalo limedumu kwa kipindi cha zaidi ya miaka miwili ikiendelea.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.

#Follow @radioonetanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *