#HABARI: Jeshi la Polisi mkoani Tabora, limetoa tuzo kwa maafisa nane wa jeshi hilo mkoani hapo waliotekeleza majukumu yao vema katika kipindi cha mwaka 2024. Ambapo kila afisa aliyepewa tuzo hiyo amekabidhiwa kiasi cha shilingi laki tano kwa lengo la kutoa hamasa kwa askari wengine kufanya kazi kwa bidii na weledi.
Aidha Jeshi hilo pia limewatunuku hati ya shukrani wadau mbalimbali waliofanikisha utendaji kazi wa polisi mkoani hapo ikiwemo chombo cha habari cha ITV ambapo hati hiyo imepokelewa leo na mwakilishi wa ITV mkoani Tabora ndugu Apollo Benjamin.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania