#VIDEO: Naibu Waziri Nishati, Mhe Judith Kapinga amesema hadi kufikia mwezi Machi 2025 takribani Shule za Serikali 216 zimehamia katika matumizi ya nishati safi ya kupikia ambapo kati ya hizo, Sekondari 146 zinatumia gesi ya LPG.
Mhe. Kapinga ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma, wakati akijibu swali la la Mbunge wa Liwale, Mhe. Zuberi Mohamedi Kuachauka, aliyeuliza ni lini majiko yanayotumia gesi yataanza kutumika kote nchini.
“Serikali kupitia REA inaendelea kutoa ruzuku ya ujenzi wa miundombinu ya nishati safi ya kupikia kwa shule nyingine na tarehe 20 Aprili, 2025, REA kupitia Wizara ya Nishati imepokea kibali kutoka TAMISEMI cha kufunga miundombinu ya huduma ya nishati safi ya kupikia katika shule 115 zikiwemo shule za Mikoa za sayansi za wasichana 16; shule za kitaifa za wavulana 7, shule za bweni za kawaida 66 na shule kongwe za sekondari 26”. Amesema Mhe. Kapinga.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania