#VIDEO: Serikali kupitia Wizara ya Madini imetoa siku 30 kwa Wamiliki wa kampuni 95 za uchimbaji wa madini kujibu hati za makosa kutokana na Wamiliki wa leseni hizo kukiuka masharti ya leseni kama yalivyoainishwa kwenye sheria ya madini kwa kutoanza shughuli za uchimbaji ambapo amesema kampuni zaba tu kati ya 95 ambazo hazijaanza uchimbaji zimelaza mtaji wa trilioni 15.
Akiongea leo Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, amesema kampuni hizo zinapaswa kujibu hoja ndani ya siku 30 lasivyo zitafutiwa leseni zao “Kama wana hoja walete majibu yao, tuyahakiki tukijiridhisha na hoja zao tutawaondolea makatazo kama hawana hoja tutawafutia leseni zao kwa mujibu wa Sheria ya Madini Sura 123 ya utoaji na ufutaji wa leseni za madini na uchimbaji kifungu cha 63 na Kanuni zake, ambacho kinaeleza ukipewa leseni unapaswa uanze kazi ndani ya miezi 18”
Amesema Serikali imetoa leseni kwa Wachimbaji wa kati na wakubwa ambazo tangu kutolewa kwake hazifanyiwa kazi “Zipo Kampuni tangu zimechukua leseni mwaka 2011 mpaka leo hazijaingiza hata koleo kwenye eneo miaka 14 sasa hazijaanza shughuli zozote, hatuwezi kuwa nchi ya namna hii, leseni 7 tu kati ya 95 ukiziweka pembeni zina mtaji wa Tsh. trilioni 15 zimelala, sisi hatuwezi kuwa nchi ambayo inatoa leseni kwa ajili ya kuchochea sekta ya madini kukua, halafu kuna Watu wanachukua leseni wanakaa nazo hawafanyii kazi kwa kisingizio kuwa tupo kwenye mazungumzo na Serikali na sababu mbalimbali”