“Mheshimiwa Spika, jumla ya kilometa 52.5 za barabara za kupunguza msongamano wa magari Jijini Dar es Salaam zimejengwa kwa kiwango cha lami. Barabara zilizokamilika ni pamoja na:
i. Barabara ya Kimara – Kibaha (19.2)
ii. Barabara ya Mabasi Yaendayo Haraka Awamu ya II kutoka Maktaba – Mbagala (km 19.3)
iii. Barabara ya Ardhi – Makongo (km 4)
iv. Barabara ya Wazo Hill – Madale (km 9).
v. Daraja la Tanzanite (km 1.03).
vi. Madaraja ya juu ya Chang’ombe na Uhasibu. Vilevile, miradi inayoendelea kutekelezwa ni pamoja na:
i. Ujenzi wa Barabara za Mabasi Yaendayo Haraka Awamu ya III kutoka Maktaba – JNIA – Gongolamboto (km 23.3);
ii. Ujenzi wa Barabara za Mabasi Yaendayo Haraka Awamu ya IV kutoka Maktaba – Morocco – Mwenge – Tegeta na Mwenge -Ubungo (km 30.1); na
iii. Maandalizi ya kuanza ujenzi wa Barabara za Mabasi Yaendayo Haraka Awamu ya V kutoka Ubungo – Bandarini, Makutano ya Tabata –Tabata Segerea na Tabata – Kigogo (km 27.6),” – Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania