#HABARI: Wananchi zaidi ya 3,000 wamepata huduma ya bure ya matibabu ya macho, katika Hospitali ya Wilaya ya Siha, mkoani Kilima…

#HABARI: Wananchi zaidi ya 3,000 wamepata huduma ya bure ya matibabu ya macho, katika Hospitali ya Wilaya ya Siha, mkoani Kilimanjaro kutoka Taasisi ya Dkt. Godwin Mollel kwa kushirikiana na Mo Dewji Foundation, huduma hizo zimehusisha upasuaji wa macho, utoaji wa dawa na miwani, na kugharimiwa kwa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 800, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha huduma za afya kwa jamii, hususan kwa wananchi wenye uhitaji mkubwa.

Akizungumza wakati wa kambi hiyo ya matibabu iliyofanyika Mei 4, 2025, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, aliwahimiza wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro na maeneo jirani kujitokeza kwa wingi ili kunufaika na huduma hizo zinazotolewa bure.

Ameongeza kuwa kambi hiyo ya matibabu ni mwendelezo wa juhudi za taasisi hizo katika kuunga mkono jitihada za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania za kuboresha huduma za afya kwa Watanzania wote, bila kujali hali zao za kiuchumi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *