#HABARI: Kamisheni ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, imetoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna Nchini ya Tanzania inavyokuza na kulinda Haki za Kiraia, Kisiasa, Kiuchumi, Kiutamaduni na Kijamii.
Hayo yamewekwa bayana na Mwenyekiti wa Kamisheni hiyo Prof. Remy Ngoy Lumbu katika kikao cha 83 cha Kamisheni ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, kinachofanyika katika makao makuu ya Kamisheni hiyo jijini Banjul Gambia ambapo Tanzania inawakilishwa na Wizara ya Katiba na Sheria kupitia Idara ya Haki za Binadamu.
Akiwasilisha taarifa ya Tanzania Wakili wa Serikali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Candid Nasua amewaeleza Wanachama wa kikao hicho kuhusu falsafa ya Rais Samia katika kuhakikisha haki za binadamu hazikiukwi ikiwa ni pamoja na Maridhiano, Ustahimilivu ,Mageuzi na Kujenga Upya Taifa ambapo kwa kupitia majadiliano na ushirikiano imechangia katika kuimarisha Haki za Binadamu, umoja wa Kitaifa, Amani pamoja na kuleta maendeleo Nchini.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania