#HABARI: Zaidi ya vijana rika balehe 1,500 wakiwemo wanawake na wanafunzi, kutoka Kata Nne za Ichenjezya, Vwawa, Mlowo na Hasanga, zilizopo wilayani Mbozi, mkoani Songwe, wameanza kunufaika na mbinu za kujikwamua kiuchumi pamoja na kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia baada ya kuwezeshwa kiuchumi na wadau wa maendeleo shirika lisilo la kiserikali la BRAC kwa kuwapatia pembejeo za kilimo, mifugo ikiwemo kuku na mbuzi pamoja na mitaji ya biashara .
Kaimu Meneja wa Shirika hilo, Bi. Ester Kadigili, amesema matokeo tarajiwa mradi huo wa BRAC maendeleo ni kuhakikisha makundi hayo yanawezeshwa kiuchumi nakufikia malengo yao huku Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Bw. Hamad Mbega, aliyefunga mafunzo hayo kando na kupongeza mkakati huo amewataka wanufaika kuwa mfano bora katika jamii kwa kutumia mafunzo na mitaji waliyopata kuwa wabunifu na waaminifu.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.
#Follow @radioonetanzania