#HABARI: Polisi nchini Kenya eneo la Kuria Magharibi Kaunti ya Migori, wamewakamata watu watatu, wanaotuhumiwa kumrushia kiatu …

#HABARI: Polisi nchini Kenya eneo la Kuria Magharibi Kaunti ya Migori, wamewakamata watu watatu, wanaotuhumiwa kumrushia kiatu Rais William Ruto, alipokuwa akiwahutubia wakazi wa eneo la Kehancha siku ya Jumapili.

Afisa wa usalama ambaye aliomba kutotajwa jina kutokana na unyeti wa kesi hiyo, alithibitisha kuwa uchunguzi unaendelea na kwamba washukiwa zaidi wanafuatiliwa.

Aliongeza kuwa matokeo ya awali yanaonesha kuwa tukio hilo, linaweza kuwa limechochewa kisiasa na pengine lilipangwa kabla ya ziara ya Rais.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.

#Follow @radioonetanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *