Chanzo cha picha, Getty Images
Dakika 16 zilizopita
Aston Villa wamefanya majadiliano ya ndani kuhusu uwezekano wa kumnunua kiungo wa kati wa Manchester City na Ubelgiji Kevin de Bruyne, 33, ambaye ataondoka Etihad Stadium msimu huu wa joto. (Sky Sports)
Leeds wanafikiria kumfukuza meneja Daniel Farke licha ya Mjerumani huyo kupata nafasi ya kurejea Ligi Kuu ya Uingereza. (Mail)
Liverpool, Real Madrid na Manchester City ni miongoni mwa vilabu vinavyomhitaji beki wa kushoto wa Bournemouth kutoka Hungary, Milos Kerkez, 21. (Sky Sports)
Unaweza kusoma
Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United wanamenyana na Chelsea na Real Madrid kuwania saini ya kiungo wa kati wa River Plate Muargentina Franco Mastantuono, 17, ambaye ana kipengele cha kuachiliwa kwa pauni milioni 38. (Mail)
Manchester United itakabiliana na ushindani mkubwa wa kutaka kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Brazil Matheus Cunha, 25, huku Arsenal na Aston Villa zikiwa miongoni mwa klabu tano za Ligi ya Premia zinazomtaka mshambuliaji huyo wa Wolves. (Sky Sports)
Nottingham Forest na Bayer Leverkusen watamlenga kiungo wa kati wa Manchester City Muingereza James McAtee mwenye umri wa miaka 22 kama City watamnunua kiungo mshambuliaji wa Uingereza Morgan Gibbs-White au kiungo mshambuliaji wa Ujerumani Florian Wirtz, 21. (Telegraph)
Chanzo cha picha, Getty Images
Winga wa West Ham wa Ghana Mohammed Kudus mwenye umri wa miaka 24 anavutiwa na Al-Nassr. (Guardian)
Al-Hilal wametuma ofa ya pauni milioni 75 ($100m) kumnunua mshambuliaji wa Barcelona Raphinha na kumpa mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 28 mkataba wa miaka minne wenye thamani ya £151m ($200m). (Sport)
Mshambuliaji wa Chelsea na Ureno Joao Felix, 25, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo AC Milan, ameanza mazungumzo ya kurejea katika klabu yake ya zamani ya Benfica msimu wa joto. (CaughtOffside)
Mazungumzo yanaendelea kati ya Barcelona na meneja wao Mjerumani Hansi Flick, 60, kuhusu kandarasi mpya hadi 2027. (Sky Germany).
Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji wa Brazil Vinicius Jr, 24, yuko katika hatua za mwisho za kuongeza mkataba wake na Real Madrid. (Fabrizio Romano)
Arsenal inasalia na matumaini ya kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Uhispania Martin Zubimendi, 26, licha ya kiungo huyo wa kati wa Real Sociedad kuhusishwa na kuhamia Real Madrid. (CaughtOffside)
Leeds United, ambayo ilipanda daraja la Ligi ya Premia siku ya Jumatatu, inaweza kumpoteza mlinzi wa Jamhuri ya Dominika mwenye umri wa miaka 28 Junior Firpo kwenda Real Betis ya Uhispania msimu huu wa joto. (Todofichajes)