Viongozi wa nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki wamefanya juhudi kwa mara nyingine za kujaribu kuleta amani mashariki mwa Jamhur ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC.
Imechapishwa:
Dakika 1

Matangazo ya kibiashara
Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki (EAC) walifanya jaribo lingine la kuleta amani mashariki mwa Kongo siku ya Jumamosi lakini, lakini matarajio yake bado hayajaonekana kufuatia mkutano wa kilele wa kikanda ambao rais wa Kongo hakushiriki na mwenzake wa Rwanda kuondoka mapema.
Viongozi walioshiriki mkutano huo ni pamoja na Salva Kiir wa Sudani Kusini, Samia Suluhu wa Tanzania, William Ruto wa Kenya,Yoweri Museveni wa Uganda na Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia.
Rais Paul Kagame aliondoka muda mfupi baada ya mkutano huo lakini hakuna maelezo yaliyotolewa kuhusu kutoshiriki kwa Felix Tshisekedi.
Taarifa iliyosomwa mwishoni mwa mkutano wa faragha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki mjini Arusha, Tanzania, imesema tu haja ya kujumuisha pamoja juhudi zote za kutafuta amani kwa ajili ya amani ya kudumu na endelevu mashariki mwa Kongo.