
Siku 500 tu baada ya Oktoba 7, baraza la mawaziri la Israeli linatazamiwa kukutana Jumatatu, Februari 17, kujadili kuendelea kwa makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza. Israeli pia aimetangaza kuwa imetuma wapatanishi huko Cairo, baada ya Waziri Mkuu wa Israeli kukutana kwa mazungumzo huko Jerusalem na Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio, baada ya kuenekana maendeleo kadhaa.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Jerusalem, Michel Paul
Kufuatia mazungumzo kati ya Waziri Mkuu wa Israeli na mjumbe wa Marekani katika Mashariki ya Kati, Steve Witkoff, ujumbe wa Israel unaelekea kwenye mazungumzo siku ya Jumatatu.
Ikumbukwe kwamba mamlaka yake ni mdogo katika kuendeleza utekelezaji wa awamu ya kwanza ya makubaliano ya kusitisha mapigano. Ni pamoja na kuingia katika Ukanda wa Gaza kwa baadhi ya nyumba 60,000 rahisi kuhamisha na vifaa vya kuandaa sehemu zitakazowekwa nyumba hizo. Kwa upande wake, Israeli inatarajia kupata kuachiliwa kwa mateka sita katika siku zijazo.
Siku ya Jumatatu hii jioni, mkutano wa baraza la mawaziri la usalama utafanyika mjini Tel Aviv kujadili awamu ya pili ya makubaliano ya amani. Kufuatia mjadala huu, maagizo mapya yanaweza kutumwa kwa wapatanishi wa Israeli ili kusonga mbele kwa hatua mpya.
Siku ya Jumapili, Benjamin Netanyahu alisema baada ya mkutano wake na Marco Rubio, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, kwamba Israel na Marekani zina mkakati wa pamoja, ambao maelezo yake yote hayakuweza kufichuliwa hadharani.
Mikutano na matangazo hayo yamekuja siku 500 baada ya mashambulizi ya kigaidi ya Hamas nchini Israeli ambayo yalizua vita. Kwa kukumbuka tarehe hiyo, familia za mateka wa Israel zilianza mfungo wa dakika 500, au takriban saa nane, ili kuweka shinikizo zaidi kwa serikali Israeli.