Israeli yataka raia kuhamishwa kwa bandari tatu za Yemen zinazodhibitiwa na Houthi

Jeshi la Israeli limetoa wito kwa wakazi kuondoka katika bandari tatu nchini Yemen siku ya Jumatatu jioni, ikiwa ni utangulizi wa mashambulizi dhidi ya miundombinu ya Wahouthi, ambayo mara kwa mara hurusha makombora dhidi ya Israeli kuwaunga mkono Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Kutokana na matumizi ya bandari za utawala wa kigaidi wa Houthi (…) tunatoa wito kwa wote waliopo” katika bandari za Ras Issa, Hodeidah, na Al-Salif “kuwahamisha mara moja na kuondoka kutoka kwao, kwa usalama wao,” ameandika Kanali Avichay Adraee, msemaji wa jeshi la Israeli, katika ujumbe wa Kiarabu uliosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ya X na Telegram.

Wahouthi, wanachama wa “mhimili wa kambi ya upinzani” unaoungwa mkono na Iranidhidi ya Israeli, wamefanya mashambulio kadhaa ya makombora na ndege zisizo na rubani dhidi ya Israeli tangu kuanza kwa vita katika Ukanda wa Gaza, vilivyoanza Oktoba 7, 2023, kufuatia shambulio la kundi la wanamfambo wa Kiislamu wa Kipalestina Hamas dhidi ya Israeli.

Takriban mashambulizi haya yote yamezuiliwa.

Waasi wa Houthi pia wameshambulia meli wanazoamini kuwa zina uhusiano na Israeli katika pwani ya Yemen, nchi iliyoko kwenye Rasi ya Uarabuni, hasa katika Bahari Nyekundu.

Mnamo Mei 4, kombora lililorushwa na Wayemen liligonga eneo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ben-Gurion karibu na Tel Aviv kwa mara ya kwanza, na kusababisha majeraha machache na uharibifu mdogo wa vifaa.

Katika kulipiza kisasi mashambulizi hayo, jeshi la Israeli lilifanya mashambulizi kadhaa katika miezi ya hivi karibuni dhidi ya malengo ya Houthi nchini Yemen, zikiwemo bandari na uwanja wa ndege katika mji mkuu, Sanaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *