Israeli yataka ‘kuondolewa kabisa kwa wanajeshi’ katika Ukanda wa Gaza

Israeli inadai “kuondolewa kabisa kwa wanajeshi katika Ukanda wa Gaza” baada ya vita, Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Gideon Saar amesema siku ya Jumanne, Februari 18, shirika la habari la habari la AFP.

Imechapishwa:

Dakika 1

Na: RFI na mashirika mengine

Matangazo ya kibiashara

Israeli imedhamiria kufikia “kuachiliwa kwa mateka wetu wote” na kufanikiwa kwa “malengo yote ya vita yaliyowekwa” na serikali, Saar amesema katika mkutano na waandishi wa habari huko Jerusalem. “Tunataka kuondolewa kabisa kwa wanajeshi huko Gaza. “Hatutakubali kuendelea kuwepo kwa Hamas au kundi lolote la kigaidi huko Gaza,” ameongeza.

Tangu Oktoba 2023, Israeli imekuwa ikiongoza mashambulizi katika Ukanda wa Gaza yenye lengo la kutokomeza Hamas. Mzozo huo unaenea katika eneo lote. 

‘Juhudi’ zinaendelea kuwakomboa mateka zaidi wiki hii

“Juhudi” zinaendelea kuhakikisha kuachiliwa kwa mateka zaidi wa Israeli wiki hii kuliko ilivyoainishwa katika makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israeli na Hamas, vyanzo vya Israeli na Palestina vimesema Jumanne.

Serikali ya Israel “inafanya juhudi kubwa” kupata kuachiliwa kwa mateka sita wakiwa hai wiki hii na kurejeshwa kwa miili ya mateka wengine wanne waliofariki, chanzo rasmi cha Israeli kimeliambia shirika la habari la AFP. Kwa upande wake, chanzo cha Kipalestina kilicho karibu na majadiliano hayo kimeripoti “juhudi” za wapatanishi kwa lengo la “kurejesha miili ya wafungwa kadhaa wa Israeli kabla ya Ijumaa” na idadi kubwa zaidi ya kuachiliwa kwa mateka moja kwa moja siku ya Jumamosi.