
Katika siku ya tatu ya mzozo kati ya Israel na Iran, Tel Aviv ilifanya mashambulizi mengine dhidi ya Iran ssiku ya Jumapili, Juni 15, 2025, kufuatia mashambulizi ya makombora ya Iran katika eneo la kaskazini mwa Israeli, na kusababisha vifo vya watu kumi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wakati wa usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili, Iran imerusha wimbi jipya la makombora huko Israeli, ikidai kuwa imelenga vituo vya uzalishaji wa mafuta ya taa na vituo vya usambazaji wa nishati, na kuua watu wasiopungua kumi. Ndege za kivita za Israeli zilishambulia maeneo yanayohusiana na kijeshi na nyuklia na maghala ya mafuta katika miji kadhaa ya Iran siku ya Jumapili, huku Benjamin Netanyahu akiahidi kuyashambulia “maeneo yote ya utawala wa Iran” na kukabiliana na “pigo la kweli kwa mpango wa nyuklia wa Tehran.”
Tangu shambulizi kubwa la siku ya Ijumaa dhidi ya Iran, mashambulizi ya Israeli yameua takriban watu 128 na kujeruhi zaidi ya 320. Pia yamewaua maafisa wa ngazi za juu zaidi wa nchi hiyo, wakiwemo viongozi wa Walinzi wa Mapinduzi. Kwa upande wa Israeli, vifo 13 na majeraha tisa makubwa yameripotiwa tangu siku ya Ijumaa, kulingana na mamlaka.
Oman imetangaza kuwa mazungumzo ya nyuklia yaliyopangwa kufanyika Jumapili, Juni 15, kati ya Iran na Marekani hayatafanyika. Iran haitajadili mpango wake wa nyuklia na Marekani ikiwa Israeli itaendelea na mashambulizi yake, rais wa Iran alionya siku ya Jumamosi, akionya juu ya jibu “kubwa” ikiwa mashambulizi ya Israeli yataendelea.