
Nchini Israeli, mazishi ya familia ya Bibas, ambao miili yao ilirejeshwa wiki iliyopita na Hamas, yatafanyika leo Jumatano, Februari 26. Maelfu ya watu wanatarajiwa kupanga foleni barabarani kutoa heshima zao za mwisho kwa Shiri, mama huyo, na wavulana wake wawili wadogo, Kfir na Ariel.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu maalum huko Jerusalem, Pierre Olivier
Msafara wa mazishi utaanzia Tel Aviv hadi eneo karibu na Kibbutz ambapo familia ya Bibas iliishi, nje kidogo ya Ukanda wa Gaza. Jukwa la familia za mateka linawataka wale wote wanaotaka kuandamana na familia ya Biba hadi kwenye mapumziko yao ya mwisho kuja kufanya hivyo bila hofu yoyote.
Katika njia nzima, maelfu ya watu wamekusanyika kutoa heshima zao za mwisho kwa wavulana wawili, Kfir na Ariel, ambao walikufa wakiwa mikononi mwa watekaji nyara baada ya kutekwa na Hamas wakiwa na umri wa miezi minane na miaka minne mtawaliwa, pamoja na mama yao Shiri, ambaye pia alifariki akiwa mokononi mwa watekaji nyara.
Mazishi haya pia yanahitimisha msururu wa dhaa na uvumi potovu kuhusu mama huyo na watoto zake. Takriban wiki moja iliyopita, siku ya Alhamisi ya wiki iliyopita, saa chache baada ya maiti hizo kukabidhiwa kwa Israeli, wachunguzi wa afya walithibitisha kwamba mwili wa Shiri haukuwa wake, ulibadilishwa na ya mkazi wa Gaza, kabla ya kuthibitisha kuwa ni mabaki yake.
Hali ambayo ilizidi kuamshahasira ya Waisraeli huku ikizidisha maumivu yaliyosababishwa na kurejea kwa miili hiyo.
Mazishi hayo, ambayo yatafanyika ndani ya mfumo madhubuti wa kifamilia, yataruhusu taifa zima kuanza maombolezo yake. Kufikia kesho, Alhamisi, miili mingine minne ya mateka waliofariki inatarajiwa kurejeshwa na Hamas kwa Israeli.