Israeli: Askari wa akiba 970 wanashutumu kuendelea kwa vita Gaza

Licha ya shinikizo kutoka kwa uongozi wa kijeshi, kundi la askari wa akiba karibu 1,000 wa Israeli wanalaani vita visivyoisha huko Gaza. Wameweka hadharani barua yao siku ya Alhamisi hii, Aprili 10. Wanadai kurejeshwa kwa mateka hata kama itamaanisha mwisho wa vita dhidi ya Hamas.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu maalum mjini Jerusalem, Aabla Jounaïdi

Magazeti kadhaa ya Israel yameripoti barua ya askari wa akiba siku ya Alhamisi, Aprili 10. Hii si barua ya kwanza ya aina hiyo. Lakini idadi – watia saini 970 – ina athari yake. Kufuatia vitisho vya kuzuia kuchapishwa kwake, makao maku ya jeshi na Wizara ya Ulinzi wameamua kuwafukuza waliotia saini ambao kwa sasa wanastahili kuhamasishwa.

Kulingana na wanajesi hawa wa akiba, vita hivi sasa vinatumika kwa “maslahi ya kisiasa na ya kibinafsi.” Mabishano mara nyingi yamesikika kutoka kwa upinzani wa kisiasa na baadahi ya ndugu wa mateka. Ofisi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu inawaelezea waliotia saini kama “wenye itikadi kali.”

Hata hivyo, barua hii haitoi wito wa kukataa kwa jumla kuhudumu, kulingana na askari waliotia saini. Inataka serikali kutoa kipaumbele kwa kuachiliwa kwa mateka kuliko kuendelea kwa vita: “Kuendeleza vita,” askari wa akiba wanasema, “kutasababisha vifo vya mateka, wanajeshi na raia wasio na hatia.” 

Wanajeshi kadhaa wa akiba walikuwa tayari wamekataa kurejea Gaza, ambapo wataalam wa Umoja wa Mataifa wamezingatia kuwa mbinu za vita za Israeli “zinaendana na sifa za mauaji ya kimbari.” Mwezi uliopita, wanajeshi wawili wa Israeli waliopinga kuanzishwa tena kwa mashambulizi ya mabomu walifukuzwa kazi na wakuu wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *