Israel yawafukuza wanaharakati waliokamatwa wakielekea Gaza

Kikundi hicho cha wanaharakati akiwemo mtetezi wa haki za binaadamu kutoka Sweden Greta Thunberg liling’oa nanga Juni mosi kutoka Italia kwenye boti ya Madleen iliyokuwa imebeba chakula na bidhaa nyingine kwa ajili ya watu wa Gaza. Vikosi vya Israel viliizuia boti hiyo Jumatatu wakati ikiwa kwenye eneo la bahari lisilo na mipaka na kuikokota hadi bandari ya Ashdod.

Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Israel imesema wanaharakati hao 12 waliwasili katika uwanja wa ndege wa Ben Gurion ili kuondoka Israel na kurejea makwao. Imesema wale watakaokataa kusaini nyaraka za kufukuzwa nchini Israel watafikishwa mahakamani.

Muungano wa Freedom Flotilla, ambalo ni kundi la uwanaharakati linaloendesha boti hiyo, lilisema wanaharakati hao wanashughulikiwa na kuhamishwa kwenye kizuizi cha maafisa wa Israel. Umesema huenda wakaruhusiwa kuondoka Tel Aviv leo usiku.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *