Israel yasema usitishaji vita wa Gaza utaisha iwapo Hamas haitawaachia huru mateka ifikapo Jumamosi

Waziri mkuu wa Israel ameionya Hamas kuwa itamaliza usitishaji vita huko Gaza na kuanzisha upya mapigano makali ikiwa kundi hilo la Palestina “halitawarudisha mateka wetu” ifikapo Jumamosi mchana.