Israel yapokea tena shehena ya makombora mazito kutoka US iliyokuwa imezuiliwa kupewa na Biden

Utawala wa Kizayuni wa Israel umepokea shehena ya mabomu mazito ya MK-84 kutoka Marekani baada ya Rais wa nchi hiyo Donald Trump kuondoa kizuizi cha uuzaji wa silaha hizo kilichokuwa kimewekwa na serikali ya mtangulizi wake Joe Biden. Hayo yamethibitishwa na Israel Katz, waziri wa vita wa utawala huo ghasibu.